} });
 


MTU mmoja ambaye hakupatikana na hatia katika shambulio la kigaidi la Westgate nchini Kenya ametekwa nyara alipokuwa akielekea nyumbani.

 

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba Liban Abdullahi Omar alikuwa ndani ya teksi na dada zake wakati watu waliojihami kwa bunduki waliposimamisha gari lao na kumteka nyara.

 

Wakili wake Mbugua Mureithi, aliliambia shirika la habari la AP kwamba watu hao walijitambulisha kama maafisa wa usalama, hata hivyo polisi imekataa kutoa tamko kuhusu tukio hilo.

 

Watu hao walidaiwa kumkamata na kumweka katika eneo la nyuma la gari lao mbali na kuchukua funguo za teksi hiyo. Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi katika mji mkuu wa Nairobi.

 

Omar ambaye ni mkimbizi wa Somalia nchini Kenya alikuwa anatoka katika kitengo cha maafisa wa kukabiliana na ugaidi mjini Nairobi wakati alipotekwa nyara kulingana na Khelef Khalifa mkurugenzi wa shirika la haki za kibinadamu la Kiislamu Muslim For Human Rights.

 

Alikuwa ameachiliwa kutoka katika jela ya kamiti na kwamba alikuwa anajaza fomu za kumwachilia huru kama ulivyo utaratibu wa washukiwa wa ugaidi katika afisi za maafisa wa kukabiliana na ugaidi.

 

Khalifa alisema kwamba watu waliosema ni maofisa usalamana waliojifunika uso kwa vitambaa vyeusi,  waliizuia teksi iliokuwa imembeba Omar.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top