} });
 


Sheikh mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakari Zubeir amewataka watanzania kuhakikisha wanailinda amani ya nchi wakati huu ambapo taifa linaelekea kufanya uchaguzi mkuu.

Shekhe mkuu ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa ujumbe wa Mufti kuelekea uchaguzi mkuu.

“Tusitumike na watu wengine kuivuruga amani yetu ambayo mwenyezi mungu ametupatia hii ni tunu ya watanzania wote bila ya kujali dini zao na makabila yao” amesema Mufti

Aidha amewasisitiza watanzania kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kwenda kumchagua kiongozi wanaemtaka

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top