} });
 


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufanya kampeni kwa siku saba.

NEC imesema imefikia uamuzi huo kwa kile ilichokiita kuwa Lissu kukiuka maadili ya uchaguzi.

Uamuzi huu umetokana na malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya NRA na Chama cha Mapinduzi (CCM),  kuwa Tundu Lissu alitoa maneno ya uchochezi.

Akiwa Mkoani Mara Lissu alisema Rais Magufuli ameitisha kikao cha wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top