} });
 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama zilizo kwenye mipaka ya nchi ziwadhibiti raia wakigeni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu. 

NEC imesema kitendo cha wageni kuingia nchini na kupiga kura ni kinyume na sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuepusha vurugu na uvujifu wa amani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ametoa agizo hilo katika kikao kati ya maosa wa tume na wadau wa uchaguzi kilicholenga kutoa elimu ya mpiga kura kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi itekeleze kwa vitendo miongozo iliyoitoa, kwa kutoa haki sawa kwa makundi yote kushiriki uchaguzi mkuu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top