} });
 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge, ametoa rai kwa wananchi wote waliojiandikisha kuwahi kwenda kupiga kura na kuendelea na majukumu ya kujenga taifa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Kunenge ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kura ni haki ya msingi hivyo wananchi watumie nafasi yao ya msingi kikatiba kupiga kura.

Aidha, Kunenge amewasisitiza wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kulinda uwepo wa amani na utulivu na ametoa onyo kwa wananchi au kikundi chochote kinachodhamiria kuhatarisha amani au kuleta vurugu wasije wakathubutu kwani jeshi limejipanga kulinda wananchi wake.

“Hakuna Mwananchi yeyote atakayebughudhiwa kutumia haki yake ya msingi” amesema Kunenge.

Amesema kuwa wananchi wawe huru kushiriki vizuri, kupiga kura na kutumia nafasi waliyoipata kutimiza haki yao ya msingi kwani siku hiyo pia itakuwa siku ya mapumziko kama ilivyotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top