} });
 

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. 

Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo alipohutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mjini Singida jana. 

"Kuna watu fulani fulani wanazungumza maneno yenye kila aina ya viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha kampeni serikali haipo kazini. Niwatahadharishe kamwe wasithubutu kufanya hivyo wataishia kwenye mkono wa sheria," alisema na kuongeza:"Mpaka mda huu serikali ipo, na Rais wetu sote bado ni Dk. John Pombe Magufuli. 

Katika hatua nyingine, 'Mama' Nchimbi alimpongeza Rais kwa ujasiri,na maono yake kwa namna ya pekee alipofanikiwa kulivusha salama Taifa dhidi ya janga hatari la Corona.

"Haya maamuzi sio mepesi mepesi tazameni nchi nyingine zinavyoendelea kuteseka mpka sasa...kwakweli tunamshukuru sana Rais na Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza na kumjalia hekima na busara ili mapenzi yake ya dhati kwa watanzania wenzake yazidi kushamiri." 

Aidha, katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), Nchimbi aliwakumbusha wazazi kuepuka kuwapa simu watoto wawapo masomoni ili kuwajengea nidhamu ambayo itakuwa ni msingi wa ufaulu na mafanikio yao kwenye tafakari ya masomo. 

Akizungumzia maisha ya wahitimu hao baada ya kidato cha nne, aliwaasa kuwa waangalifu na kuepuka mitego na vishawishi vya kidunia ambavyo vinaweza kuwatumbukiza katika mashimo ya dhambi na kuharibikiwa, ikiwemo kupoteza ndoto zao njema za maisha walizonazo. 

Kwa upande wake, Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi aliwataka wahitimu hao kutafakari sambamba na kuchukulia mahafali hayo na malezi waliyopewa kwa kipindi chote kama kiapo chao kwa Mungu cha kutotenda dhambi wala kurudia kutenda dhambi na wasisahau kila mmoja kuendelea kulinda usafi wa moyo popote pale watakapokuwepo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top