} });
 

Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera, aliwasili nchi Tanzania Oktoba 7, 2020 kwaajili ya ziara ya kitaifa ya siku tatu lakini alikatisha ziara hiyo na kurejea nchini kwakwe mapema, ambapo aliondoka oktoba 8, 2020 akipunguza siku moja katika ziara yake.

Ikulu ya Malawi imesema kuwa kiongozi huyo alikatisha ziara yake na kurejea nchini humo kwani alitakiwa kushughulikia mambo kadhaa ya haraka ya ndani ya nchi.

Rais Chakwera, anatarajiwa kuhudhuria maandamano yaliyoandaliwa na wanawake kupinga kukosekana kwa usawa wa kijinsia yanayofanyika leo.

Hata hivyo wanawake hao wanaandamana kufuati Rais Chakwera, kushindwa kutimiza takwa la kuhakikisha uteuzi wake katika ofisi za umma unazingatia usawa wa kijinsia 60-40.

Itakumbukwa Rais Chakwera, katika hotuba yake ya jumatatu ya kuadhimisha siku 100 madarakani alisema anahitaji muda zaidi kufanikisha takwa hilo.

Akiwa nchini Tanzania Rais Chakwera, alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli, kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, lakini pia alishiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye stedi mpya ya kimataifa ya mabasi ya mikoani na nje ya nch Jijini Dar es Salaam.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top