} });
 


Mkuu Wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge Oktoba 2 amezindua safari ya kwanza ya treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Arusha, baada ya karibu miaka 30 ya kusitishwa kwa usafiri wa treni ya Dar es Salaam hadi Arusha.

Akizindua safari hiyo RC Kunenge amelielekeza Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri na kuwapongeza Kwa mapinduzi makubwa na mazuri wanayoyafanya kwenye usafiri wa  reli.

Aidha, Kunenge amesema treni hiyo itasaidia wafanyabiashara na  wananchi hususani wa kipato cha kawaida kupata usafiri Wa haraka na Kwa bei nafuu hivyo ametoa wito Kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake Mkurugwnzi Mkuu wa TRC mhandisi Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limejizatiti vyema kuhakikisha linatoa huduma bora na salama kwa wananchi wote.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top