} });
 

Simba SC ndio timu iliyofunga magoli mengi ligi kuu Tanzania bara msimu huu magoli 14 katika michezo 5

Simba SC, Yanga SC na Azam FC zimeendeleza ubora kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu, ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja.

Ligi kuu Tanzania bara imefika raundi ya 5 na baada ya kumalizika kwa kalenda ya kimataifa ya FIFA raundi ya 6 itarejea tena Oktoba 14, mpaka sasa imechezwa michezo 45.

hizi ni baadhi ya takwimu baada ya michezo ya raundi ya tano katika msimao wa ligi kuu.

Katika michezo 5 ambayo kila timu imecheza mpaka sasa ni timu 3 tu ambazo hazijafungwa mchezo hata mmoja,

Timu hizo ni Azam FC ambao wameshinda michezo yao yote na ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 15, Simba SC wameshinda michezo 4 na wametoka sare mchezo mmoja wanajumla ya alama 13 wakiwa nafasi ya pili,

Timu nyingine ni Yanga nao hawajapoteza mchezo wameshinda michezo 4 na wametoka sare mchezo mmoja wakiwa nafasi ya 3 na alama 13.

Azam FC ndio timu pekee iliyoshinda michezo yote 5 ya ligi kuu, na wanaongoza ligi wakiwa na alama 15

Ihefu na Mbeya City ndio timu zilizopoteza michezo mingi 4 kila timu, Mbeya City ndo timu pekee ambayo haijashinda mchezo hata mmoja, katika michezo 5 wamefungwa michezo 4 na wametoka sare mchezo mmoja na wanaburuza mkia katika msimamo.

Wakati Ihefu wameshinda mchezo mmoja wamefungwa michezo 4 wapo nafasi ya 17 na alama zao 3 kwenye msimamo.

Yamefungwa mabao 74 katika michezo hiyo 45 ambao ni wastani wa bao 1.644.. kwa mchezo, Simba SC ndio timu iliyofunga mabao menge wamefunga jumla ya mabao 14 wakiwa na wastani wa kufunga goli 2.8 kwa mchezo, wakifatiwa na Azam FC waliofunga mabao 9 na wastani wao wa kufunga kwa mchezo ni bao 1.8.

Klabu ya Manisapaa ya Kindondoni KMC wanashika nafasi ya tatu wakiwa wamefunga mabao 8 na wastani wao wa kufunga kwa mchezo ni bao 1.6 nafasi ya 4 ni Yanga wakiwa na wastani wa kufunga bao 1.4 kwa mchezo kwani mpaka sasa wamefunga mabao 7kwenye michezo 5, timu ya tano ni Polisi Tanzania wamefunga mabao 6 na wastani wao wa kufunga kwa mchezo ni 1.2.

JKT Tanzania ndio timu iliyofungwa mabao mengi 8 mpaka sasa kwenye ligi wakifatiwa na Mbeya City na Ihefu ambao wote kwa pamoja wameruhusu mabao 7.

Simba ndio timu iliyokusanya alama nyingi katika viwanja vya ugenini katika michezo 3 ya ugenini wameshinda michezo 2 na wametoka sare mchezo mmoja, wamekusanya alama 7 kati ya 9.

Yanga na Azam FC zinafatia zote zimeshinda michezo miwili waliocheza ugenini, wakiwa wamekusanya alama 6 kila timu. Polisi Tanzania nayo imekusanya alama 6 katika michezo 3 ya ugenini wameshinda michezo miwili na wamefungwa mchezo mmoja.

Azam FC, Biashara United, Simba SC na Dodoma Jiji Fc ndio timu zilizoshinda michezo yote waliocheza katika viwanja vyao vya nyumbani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top