} });
 

 

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wameondoka leo Ijumaa, Oktgoba 02 kuifuata JKT Tanzania, jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara amesema sababu ya Simba kutumia Basi kwenda Dodoma tofauti na utaratibu wao wa kutumia ndege Ni kutimiza maombi ya mashabiki wao wa Morogoro ambao wameomba wapelekewe taji la ligi.

“Kikosi kimeondoka kwa basi kuelekea Dodoma na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutimiza ombi la mashabiki wa Morogoro ambao waliomba tuwapelekee taji letu la ligi ambalo tulitwaa msimu uliopita”.

“Hivyo kwa kukubali ombi letu la mashabiki wa Morogoro tutakuwa na kombe letu, mashabiki watapata muda wa kuliona kombe letu na kesho Jumamosi tutaendelea na safari kuelekea Dodoma ambapo tutapata muda wakufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuikabili JKT Tanzania,” amesema Haji Manara.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top