
Tanzania na China zimekubaliana kuendeleza mahusiano ya kimkakati baina yao ili kuwezesha
uwepo wa ulingo sawa miongoni mwa mataifa katika kusimamia maslahi na maendeleo ya nchi
husika katika jumuiya za kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi
ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China
hapa nchini Mhe. Wang Ke na kusisitiza umuhimu wa Mataifa kuheshimiana na kutokubali
kuingilia uhuru wa mambo ya ndani ya nchi kwa kisingizio cha haki za binadamu,demokrasia
ama jambo lolote jingine.
Ameongeza kuwa mazungumzo hayo ya kimkakati yalilenga pia kutambua kuwa mwaka huu ni
mwaka wa 55 tangu Tanzania na China zisaini mkataba wa uraki ambao uliweka msingi wa
mahusiano makubwa na ya dhati katika nyanja za ulinzi na usalama,afya,kilimo, elimu na
miundo mbinu ambapo mpaka sasa China ni Taifa linaloongoza hapa nchini kwa uwekezaji wa
moja kwa moja.
Kwa upande wake Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Wang Ke amesema China wakati wote ni
Raki mwaminifu na wa kudumu wa nyakati zote kwa Tanzania na kwamba kutimiza miaka 55
ya uraki wa nchi hizo ni kielelezo tosha na siku zote wataendelea kuuheshimu na kuuenzi
uraki huo.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment