} });
 


Rais wa Marekani ,Donald Trump amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.


Akitoa tangazo hilo kupitia mtandao wa Twitter Trump ameandika “Usiku huu , @FLOTUS (mke wa Trump) na Mimi vipimo vimebaini tumeambukizwa Covid-19 . Wakati huohuo, tutaanza mchakato wa kuwa kwenye karantini. Tutapita pamoja katika hili”.

Taarifa hiyo inakuja siku chache baada ya msaidizi na mshauri wake Hope Hicks, 31, kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.

Bado haijafahamika kama kuthibitishwa kwa Bwana Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais, ambao umepangwa kufanyika Oktoba 15 huko Miami, Florida.soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top