} });
 

 

Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kama atapata ridhaa ya kuiongoza nchi atahakikisha anajenga nchi yenye uhuru ili wananchi waendeshe maisha yao bila kubugudhiwa.

Akizungumza Oktoba 12,2020, katika kampeni zake zilizofanyika Nzega, mkoani Tabora, amesema kuwa ili wananchi hao wapate maendeleo ya uhuru na haki inawapasa kuchagua chama hicho kiingie madarakani ili waweze kupata maendeleo.

”Tujenge nchi ya watu ,huwaliohururu kusema na kuendesha maisha yao bila kubugudhiwa na kutenda haki kwa kila mmoja wetu” amesema Tundu Lissu.

Aidha, Lissu amewaomba wananchi wa wilaya ya Igunga kuchagua baraza la madiwani litakaloongozwa na CHADEMA, kwa kuwa kwenye Halmashauri ni muhimu katika kuleta maendeleo .

‘Kwenye uchaguzi mkuu huu chagueni baraza la madiwani litakaloongozwa na  CHADEMA, kwa sababu kwenye halmashauri ni muhimu hela za maendeleo yenu wekeni kwenye halmashauri ya CHADEMA ili mambo yaende,” ameongeza Lissu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top