} });
 

 

Rais Dkt. John Magufuli ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amewaomba watanzania kutumia siku tatu kuanzia leo kumuomba Mungu virusi vya Corona viondoka nchini Kenya.

Ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2020, katika mkutano wa kampeni za kuomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Stadium Jijini Dar es Salaam.

Aidha amesema kabla hajafika uwanjani hapo amezungumza na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye amemwambia kuwa wakenya watafanya maombi ya siku tatu kuanzia leo ili Covid 19 iishe nchini humo kama ambavyo imeisha Tanzania.

“Ninawaomba ndugu zangu Watanzania tushirikiane katika maombi haya na wenzetu wa Kenya ili ugonjwa wa Corona uondoke Kenya kama Mungu alivyouondoa hapa Tanzania, na nina uhakika atatusikia”

Hadi Oktoba9, 2020 visa ziadi ya 40,0000 vimeripotiwa nchini Kenya ambapo watu zaidi ya 26,300 wamepona huku waliofariki wakiwa ni 751.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top