} });
 

Mfano wa picha ya chemba inayotoa maji machafu

Wakazi na wafanyabiashara wa eneo la Ubungo National Housing, wameiomba serikali kuziba chemba inayotoa maji machafu kwani imekuwa ikisababisha uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya zao kutokana na eneo hilo huwa pia linatumika kwa ajili ya biashara ya chakula.

Wakizungumza Novemba 21, 2020 wamesema eneo hilo limezungukwa na wafanyabiashara wa chakula hivyo uwepo ubovu wa chemba unapelekea ukosefu wa wateja kutokana na harufu mbaya inayotoka katika chemba na kuongeza kuwa washametoa taarifa kwa serikali ya Mtaa na  DAWASCO lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilichokuliwa.

Aidha wameongeza kuwa chemba hiyo imebomoka  kwa  muda mrefu hali inayowatia hofu wakazi hao ambapo pia wamedai kuwa chemba imekua inaleta shida mara kwa mara japo viongozi wamekuwa hawalifuatilii kwa makini tatizo hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top