} });
 

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amehaidi kufanya maboresho miundombinu ya barabara zilizopo kwenye Kata ya Ngamiani Kati ili kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ambazo wanakumbana nazo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngamiani Kata wakati wa mkutano wake wa kampeni ambapo barabara hizo ni kuanzia barabara ya tisa mpaka kumi na nne

Alisema kwamba amekusudia kuzifanyia maboresho barabara hizo ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto zilizopo kwa sasa za baadhi yao kutokuwa na miudombinu mizuri.

Akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kusikiliza sera zake alisema pamoja na kuboresha barabara hizo atasukuma pia ujenzi wa miundombinu rafiki ya kupitisha maji ili kuzuia mafuriko.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto alisema pia mipango yake ni kuanzisha ujenzi wa soko la Ngamiani hususani kwa upande wa Samaki.

 Katika hatua nyengine Ummy alimuombea kura Mgombea Urais wa Dkt John Magufuli ambae katika awamu ya kwanza ya miaka mitano Serikali yake imejenga miundombinu ya kutosha katika sekta ya Afya.

“Lakini pia katika awamu ya pili imedhamiria kuimarisha bima ya Afya ili wananchi wengi waweze kupata huduma ya Afya pasipo vikwazo”Alisema


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top