} });
 

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ,Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa kuelekea mzunguko wa sita wa kampeni, chama hicho kimejipanga kufanya mikutano minne katika jiji la Dar es salaam.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho uwanja wa Taifa wa Mkapa amesema lengo la ratiba hiyo ni kuwafikia wananchi wote wa jiji la Dar es Salaam .

“Hapa tumekusudia kuwafikia wapiga kura wa majimbo ya Mbagala, Temeke na Kigamboni, mkutano wa pili utakuwa Kinyerezi wa tatu utakuwa Mburahati na wa mwisho utakuwa Tanganyika Pakers kwa majimbo ya Kawe na Kinondoni,”amesema Bashiru.

Aidha amesema kuwa CCM itaendelea kulinda misingi ya uhuru Taifa na kutokuingia kwenye mfarakano kama alivyoagiza mwenyekiti wa chama hicho Dkt. John Magufuli .

“Sasa tunaenda kwa mtindo wa bandika bandua na tumekubaliana katika kuelekea mwisho wa kampeni tuzingatie yale ambayo ulituelekeza, kwamba kuhakikisha misingi ya uhuru wa Taifa letu”.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top