} });
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge (kulia) akiweka karatasi ya kura ndani sa sanduku la kupigia kura katika kituo cha Shule ya Msingi Kawe “A”.

ZOEZI la kupiga kura likiwa linaendelea  katika maeneo mbalimbali kote nchini watu mbalimbali katika maeneo yao wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura tangu asubuhi ya leo Oktoba 28, 2020 ambapo wananchi wanachagua viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya kuwatumikia kwa kipindi cha mhula mwingine wa miaka mitano.

 

Katika jiji la Dar es Salaam nako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge mapema leo amepiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Kawe “A” ambapo baada ya kupiga kura amezungumza na wanahabari na kuwaeleza kuwa wananchi wa mkoa wake kujitokeza kupiga kura kwani hadi sasa hakuna tukio lolote ambalo limeripotiwa la uvunjifu wa amani na hivyo kwamba Dar es Salaam ipo Shwari licha ya changamoto ndogondogo ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inazishughulikia ili kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura apate haki yake ya msingi ya kikatiba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top