} });
 

Mhandisi Mkuu wa Mkoa TANESCO Kinondoni Kaskazini Goodlove Mathayo

 
Watanzania wametakiwa kuacha kuwatumia mafundi wasio na vigezo maarufu 'vishoka' katika marekebisho ya umeme na ufungaji wa nyaya 'wiring' ili kuepuka ajali mbaya zinazoweza kuzuilika.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar Es Salaam na Mhandisi Mkuu wa Mkoa TANESCO Kinondoni Kaskazini Goodlove Mathayo katika  wiki ya maadhimisho huduma ya wateja kanda ya Dar Es Salaam

"Wananchi wanapaswa kujua fomu za kujiandikisha zinatolewa bure, survey pia ni bure na suala la wiring inabidi lifanywe na fundi wanaotambulika na EWURA" alisema Goodlove Mathayo

"Hata hivyo tunawaomba wananchi ushirikiano wao na uelewa wanapotuona mitaani tunakata katika utendaji kazi wetu inabidi watuelewe maana kuna wakati nyaya huwa zinagusana na miti na kuleta madhara au transformer kuanguka" ameongeza Mathayo

Kwa upande wake Meneja Uhusiano Shirika la  Umeme nchini TANESCO Johary Kachwamba amesema Shirika hilo limejidhatiti kuwafikisha kwenye mikono ya sheria watu wote wanaoshiriki matumizi ya umeme kwa njia ya magendo

Aidha, akiongea kwa niamba ya wananchi Mwenyekiti wa mtaa wa Kinondoni block49 amesema wiki ya huduma imekuwa na tija kwao na pia amewaomba TANESCO kurahisha mawasiliano ya dharula ili kuwafikia wateja kwa wepesi mara wanapopata na dharura

Wiki ya huduma kwa wateja kwa mkoa wa kikanda wa Kinondoni umekamilika hii leo ambapo zaidi ya wateja 400 wamefaidika na oparesheni hiyo iliyo na lengo la kuwafikia wananchi popote walipo

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top