
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt.Charles Msonde amesema Jumla ya watahiniwa 1,024,007 wanatarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza darasa la 7 ambayo inatarajiwa kuanza kesho Oktoba 7 na 8 nchi nzima.
Dkt.Charles Msonde amewataka wasimamizi kufanya kazi yao kwa uadilifu na kulinda haki ya watahiniwa.
"Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa, kufanya kazi yao kwa uadilifu wa hali ya juu na wahakikishe wanalinda haki ya watahiniwa wenye mahitaji maalum"- Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Charles Msonde.
Pia Dkt.Msonde amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote ile kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment