Shirika
la Umoja wa
Mataifa la
Mpango wa Chakula Duniani
(WFP) nchini Tanzania limempokea mwakilishi wake mpya,
Sarah Gordon-Gibson.
Mwakilishi huyo aliwasilisha nyaraka za utambulisho kwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Profesa Palamagamba Kabudi jana Jumatano Oktoba 21, 2020.
Gordon-Gibson anachukua nafasi na mtangulizi wake, Michael
Dunford aliyeondoka Tanzania Julai, 2020 baada ya kumaliza
muda wake.
Taarifa iliyotolewa na WFP jana ilisema Gordon-Gibson
aliyekuwa naibu mwakilishi wa nchi za Tanzania, Myanmar na
Niger amefurahia kurudishwa Tanzania akisema ni nchi
iliyopiga hatua katika maendeleo.
“Tunaendelea kudhamiria kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika kukabiliana na changamoto zake za kitaifa hususan
mazingira, tabia ya nchi, skimu za kinga ya jamii, uzalishaji
katika kilimo na mifumo ya chakula, mlo kamili na lishe bora na
pia usawa na uwezeshaji wanawake,” alieleza.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Gordon-Gibson, ambaye ni
mwanasheria kitaaluma amefanya kazi na WFP kwa zaidi ya
miaka 20.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment