} });
 

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Boshu Kulwa (60) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Magdalena Lunguya (45) baada ya kumhoji kuhusu fedha za mauzo ya mbuzi.

Kamanda wa Polisi Shinyanga, Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi Msalala, kufuatilia suala hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya upelelezi kukamilika.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamingu, Masesa Manyanda amesema tukio lililokea Saa 9:00 alfajiri Novemba 5, 2020 katika kijiji cha Nyamingu, kata ya Busangi wilayani hapa.

“Nilipofika nyumbani kwao nilikuta amelazwa chumbani akiwa na majeraha mwilini, sikio la kushoto likiwa limekatwa na kitu chenye ncha kali na shingo imenyongwa,” Manyanda

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top