} });
 

 

MKUU wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, amesema serikali inaendelea kumtafuta kijana anayedaiwa kukimbia na sanduku la kupigia kura wiki iliyopita katika Kata ya Madangwa, Jimbo la Mtama ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.

 

Ndemanga alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kuthibitisha kuwapo kwa tukio la kijana ambaye hata hivyo hakumtaja jina, kupora moja ya masanduku ya kupigia kura na kutokomea nalo kusikojulikana.

 

“Ni kweli tukio la kuporwa kwa sanduku moja la kupigia kura kati ya matatu yaliyokuwapo kwenye kituo limetendeka,” alisema Ndemanga. Alisema wanaendelea kumsaka kisha kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

“Tayari taarifa zake tunazo na tunakuhakikishieni ndugu waandishi muda si mrefu atatiwa mikononi,” alisema.

 

Ilidaiwa kuwa kijana huyo alifika kituoni hapo na kupiga kura na alipomaliza kutumbukiza shahada katarasi yake, alipora sanduku lenye kura za udiwani kisha kutokanalo nje na kupanda pikipiki na kutokomea nalo kusikojulikana. Huku ndani yake likiwa na kura kadhaa zilizoshapigwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top