} });
 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha jela na kumchapa viboko sita, mkazi wa Mtaa wa National Housing, Juliasi Katambi (65), baada ya kukutwa na hatia ya kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka sita ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi.  

Akitoa hukumu hiyo hivi karibuni, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Gladness Badha alisema kuwa, kutokana na ushahidi usioacha shaka, mahakama hiyo imeridhia kumpa adhabu hiyo Katambi ili kutumikia kifungo hicho baada ya mashahidi watano kutoa ushahidi juu ya tukio hilo la ubakaji.

  

Hakimu huyo alisema kuwa, kutokana na kitendo hicho cha kinyama, mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwake na kwa jamii hasa kwa watu wenye kuendekeza vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto wa kike na wanawake.

  

Awali, Wakili wa Serikali, Peter Utafu aliieleza makahama hiyo kwamba, mnamo Aprili 22, mwaka 2019, muda wa jioni katika maeneo ya shule hiyo ya msingi iliyopo Nzega Mjini, mwanafunzi huyo alibakwa kwa nguvu na Katambi mwenye umri wa miaka 65 na kumsababishia maumivu makali kwenye mwili wake.

  

Wakili huyo alisema kutokana na kitendo hicho na upelelezi kukamilika na mashahidi watano kutoa ushahidi wa kuridhisha mahakamani hapo, ni vyema mahakama ikatoa adhabu kali kwa Katambi ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.

  

Mahakama ilitoa nafasi ya utetezi kwa mshitakiwa huyo baada ya kupatikana na hatia ambapo aliomba kupunguziwa adhabu kwa vile ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo na vilevile ana umri mkubwa.

 

Hata hivyo, Mahakama ya Wilaya ya Nzega haikuridhika na utetezi huo na kumhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela na kuchapwa viboko sita.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top