} });
 


Rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuzindua timu yake ya usalama wa taifa, akiitengeneza timu ya maafisa waliohudumu chini ya utawala wa Obama kuashiria kuwa anaondokana na sera za utawala wa Trump za Marekani Kwanza na kuurejesha mchango wa Marekani katika jukwaa la kimataifa. 

Waziri wa zamani wa mambo ya nje, John Kerry atachukua wadhifa wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Kerry na watu kadhaa wanatarajiwa kujiunga na serikali mpya itakayojadiliwa leo na Biden na Makamu wa rais mteule Kamala Harris. 

Biden anatarajiwa kumteua Janet Yellen kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya fedha. Aliteuliwa na Rais Barack Obama kuiongoza Benki Kuu ya Marekani akiwa mwanamke wa kwanza katika wadhifa huo. 

Idara ya serikali ya Marekani inayoratibu shughuli ya kubadilishana madaraka, imempatia idhini Biden ya kuendelea mbele na mchakato wa kukabidhiana madaraka.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top