} });
 

 

Kundi la Boko Haram la Nchini Nigeria limewaua  Wakulima 43 wa Jimbo la Borno katika mashamba yao ya mpunga yaliopo Zabrmari.


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kupitia Ukurasa wake wa Twitter ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho, pia amelaani mauaji hayo. Amesema kuwa, Serikali ya Nigeria imefanya yote yanayowezekana kulinda nchi hiyo na watu wake.


Aidha, Shirika la Kimataifa La kutetea  Haki za Binaadamu, Amnesty International limelaani kitendo hicho.

 

Boko Haram mara kwa mara wamekuwa wakifanya mashambulizi kwa raia ikiwa sehemu ya kushinikiza kuachiwa wajitawale Kaskani mwa Taifa hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top