} });
 

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amesema kuwa malengo yao kama wachezaji msimu huu ni kuhakikisha wanaipatia ubingwa timu hiyo.

 

Yanga msimu huu imeanza ligi kwa kishindo ikiwa ni timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kati ya michezo nane waliyocheza ambapo wameshinda michezo saba na kutoa sare mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Fei Toto alisema kuwa msimu huu malengo yao ni kuhakikisha wanaipatia Yanga ubingwa mara baada ya kukosa ubingwa huo kwa misimu mitatu, jambo ambalo wanaamini litakuwa zawadi kubwa kwa mashabiki wao.

 

“Tunafahamu kuwa mashabiki wa Yanga wana kiu kubwa ya ubingwa msimu huu na sisi kama wachezaji tumeweka malengo ya kuhakikisha tunatwaa ubingwa ili kuwapa zawadi hiyo na kama wachezaji tutahakikisha tunaupambania ubingwa.

 

“Msimu huu ligi inaonekana kuwa ya ushindani kuliko msimu uliopita na hii ni kutokana na timu nyingi kujipanga kwa kufanya usajili makini, kwa kulitambua hilo, ni lazima tuheshimu kila mchezo uliopo mbele yetu ili tupate pointi za kutufanya kuwa mabingwa,” alisema kiungo huyo.

 

Yanga, kwenye msimamo wa ligi wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 22, saw ana Azam FC ambao wanaongoza kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top