} });
 

 

EDEN Hazard ingizo jipya ndani ya Real Madrid ya Uhispania amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu  kujiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu wa mwaka jana 2019 akitokea Klabu ya Chelsea ya Uingereza.


Mbelgiji huyo alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba huku lile la pili likiwa ni la kujifunga kutoka kwa mchezaji wa Inter Milan, Achraf Hakimi, dakika ya 59.


Inter Milan ilikubali kufungwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani, Uwanja wa San Siro na kuifanya ipoteze jumla ya mechi mbili na kuwa na sare mbili kati ya mechi nne ilizocheza ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Kwenye msimamo wa kundi B ipo nafasi ya nne na Madrid wao wapo nafasi ya pili na pointi zao kibindoni ni saba. Tangu ajiunge na Madrid hajawa kwenye ubora wake kutokana na kusumbuliwa na majeraha, jambo ambalo limekuwa likimweka nje ya uwanja muda mrefu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top