} });
 


RAIS wa Iran, Hassan Rouhani, amesema lazima walipize kisasi baada ya mwanasayansi wao wa  nyuklia, Mohsen Fakhrizade, kuuawa huku wakiamini taifa la Israel kuhusika na mauaji ya mtaalamu huyo.

 

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, amesema kuna ushahidi unaoashiria uhusika wa Israel katika mauaji hayo,   Fakhrizade, 63, alikuwa mwanachama wa kikosi cha walinzi wa kimapinduzi cha Iran na alikuwa mtaalamu wa uzalishaji wa makombora ya nyuklia.  Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hii ndiyo sababu shirika la kijasusi la Israel  (Mossad) kwa muda mrefu lilitaka kummaliza mwanasayansi huyo.Mwaka 2015, makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na mataifa makubwa yaliweka ukomo wa uzalishaji wa madini hayo ya urani, lakini Rais wa Marekani, Donald Trump, alijiondoa katika makubaliano hayo miaka mitatu baadaye.

 

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden, ameahidi kuirejesha Marekani kwenye makubaliano hayo ingawa wachambuzi wanasema atakabiliwa na changamoto kubwa kulifanikisha lengo hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top