} });
 

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , wakati alipomjulia hali msanii huyo anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Novemba 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera.

Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa Novemba 08, 2020 amemtembelea na kumjulia hali mwanamziki mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii, Nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ally, Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Majaliwa alimpa pole Kikii anayesumbuliwa na matatizo ya Mgongo na amemtakia pona ya haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Aidha, Mhe. Majaliwa pia alimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.

Akizungumza na Mhe. Kasanda, Mhe. Majaliwa alimtakia pona ya haraka ili aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia WanaKatavi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top