} });
 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Dk.Bashiru Ally, amewataka viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika ngazi za Udiwani,Ubunge na Wawakilishi kuzingatia nidhamu ya chama na uwajibikaji.

Akizungumza Novemba 01, 2020, Dk. Bashiru, amesema kuwa wanao mfumo kwenye jumuiya zao za chama na kamati za siasa za ngazi zote ambazo zitasimamia na kudai kuwa deni walilonalo ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

''Kwa mara ya kwanza chama chetu kimeingia na kumaliza uchaguzi kikiwa na umoja na mshikamano tukiwa tunaheshimiana na kusimamiana niwaombe wana CCM, wasianze kusherehekea ushindi huu kana kwamba kazi imeisha ila kiukweli kazi ngumu imeanza'',amesema Dk. Bashiru Ally

Aidha amesema siri kubwa ya ushindi walioupata ni umoja wao na kuongeza kuwa ushindi huo ni kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika miaka mitano iliyomalizika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top