} });
 

Baada ya jana Novemba 07, 2020, mgombea urais wa Chama Cha Democratic, Joe Biden, kutangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Taifa la Marekani, akimshinda Rais aliyekuwa madarakani Donald Trump, Biden amesema kazi itakuwa ngumu lakini ataifanya kwa nguvu zote.

Biden ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika, ''Marekani nashukuru kwa kunichagua kuongoza taifa letu zuri, natambua kazi itakuwa ngumu ila naahidi nitakuwa Rais wa wote, walionipigia kura na ambao hawajanipigia''.

Joe Biden ambaye anakuwa Rais wa 46 wa Marekani, aliongeza kuwa, ''nitaulinda huu uaminifu mkubwa mliopatia''.

Aidha katika mahojiano na vyombo mbalimbali Rais huyo mteule wa Marekani alieleza furaha ya ushindi wake wa kihistoria katika uchaguzi wa Rais.

'Tumeshinda kwa kura nyingi kuwahi kupigwa kwa mgombea wa Urais kwenye historia ya taifa hili, kura milioni 74. Ninaahidi kuwa Rais wa Marekani na sio wa majimbo ya Bluu au Nyekundu na Marekeani itakuwa na heshima tena''.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top