} });
 

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze, amesema kuwa aliwatambua wapinzani wake ni wazito, jambo lililomfanya atumie wachezaji wenye spidi mwanzo-mwisho.

 

Mchezo huo ulikamilika kwa Azam FC kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha jumla ya pointi tatu ikiwa kwenye ngome yake ya Azam Complex.

 

Deus Kaseke alifunga bao la ushindi dakika ya 48 lililodumu mpaka dakika ya 90 na kuifanya ikwee nafasi ya kwanza baada ya kufikisha pointi 28.

 

Kaseke aliipandisha timu yake hadi nafasi ya kwanza kwa kuishusha Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba.

 

Kaze amesema:”Ilikuwa ni mchezo ambao unahitaji ushindani mkubwa na wachezaji wenye spidi kubwa ili kuwachosha wachezaji wa timu pinzani kwa sababu wao wengi ni wazito.

 

“Sasa nilipaswa kuwa na mbinu ambayo ingenipa matokeo nikaanza na Kaseke ambaye alifunga bao na kutupatia pointi tatu, katika hilo ninawapongeza wachezaji wote kiujumla pamoja na mashabiki,”.

 

Yanga  imecheza jumla ya mechi 12 ambazo ni dakika 1,080 bila kufungwa huku Azam FC ikipoteza jumla ya michezo mitatu baada ya kucheza mechi 12 na ipo nafasi ya pili.

 

Ikiwa nafasi ya tatu, Simba na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 11 imepoteza mechi mbili  ilizofungwa na Tanzania Prisons bao 1-0 na Ruvu Shooting bao 1-0.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top