
WATEMBEA kwa miguu mchana jana Jumatatu, Novemba 16, 2020, wakipita kando na mto Msimbazi jijini Dar es Salaam walikumbwa na taharuki baada ya kuona maiti ya mtoto mchanga akiwa kwenye mfuko uliotupwa hapo.
Mjumbe wa mtaa huyo alisema mapema asubuhi ya jana hiyo alipigiwa simu na watu akipewa taarifa ya kichanga hicho kutupwa kwenye mto huo.
Jeshi la polisi liliuchukua mwili huo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment