} });
 


MWILI wa kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30 na 35 umekutwa ukining'inia kwenye tawi la mti wa mwembe akidaiwa amejinyonga kwa kutumia shuka.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga alisema mwili wa kijana huyo ulikutwa maeneo ya Mlimani City kata ya Uwanja wa Ndege manispaa ya Mpanda na kwamba jina lake halikuweza kufahamika mara moja.

Alisema Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazi Mmoja, Musa Buteme (38) aliuona mwili wa huyo ukining'inia kwenye tawi la mwembe akiwa amenyongwa kwa shuka nyeupe. Alisema mwili huo ulionekana Novemba 24 mwaka huu saa 1.45 asubuhi maeneo hayo ya Mlimani City.

"Mpaka sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali teule ya rufaa mkoa wa Katavi ukisubiri utambuzi wa ndugu zake," alisema.

Kamanda Kuzaga alitoa wito kwa jamii iwatumie viongozi wa dini, kimila, na serikali katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ili kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kufanya uamuzi sahihi yatakayozisaidia familia na taifa kwa ujumla.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top