
Wafanyakazi wa huduma ya uokozi nchini Guatemala wanaendelea kufukua matope na vifusi kwa lengo la kuwatafuta watu wanaokadiriwa kufikia 100, ambao inaaminika wamefukiwa, baada ya kutokea mvua kubwa iliyoambatana na maparomoko ya ardhi.
Jitihada hizo zinaendelea wakati pia kimbunga kikali kilichopewa jina la Eta kikiendelea kukusanya nguvu zake katika muelekeo wa Cuba na kusini mwa Florida.
Nchini Guetemala, ambako watu 15 wamethibitika kufariki dunia, bado jitihada za kuwasaka wengine wanaokadiriwa 109 inaendelea.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment