} });
 


KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kuwa leo atakuwa na kazi ngumu kwani kucheza na Manchester City huwa kuna ugumu kati yao. Leo Jumapili, Man City itavaana na Liverpool kwenye Uwanja wa Etihad ukiwa ni mchezo wa Premier.

 

Msimu uliopita kwenye Uwanja wa Etihad, Man City aliibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku walipokutana Anfield, Liverpool alishinda 3-1.“Aina ya mechi hii huwa ni ngumu, lakini pia huwa nafurahia mchezo wa namna hii kwani huwa nafanya maandalizi lakini mambo yanakuja kuwa magumu yaani kukutana na Man City ni mechi ngumu kwangu kwenye soka kuliko zote. 

 

“Inakuwa mechi nzuri nimefanya maandalizi lakini unakuta napoteza au wakati mwingine nashinda ila ndiyo soka na inabidi tu ufurahi sababu huna namna.“Pamoja ni kupata changamoto na kujiandaa tumekuwa hatuchezi mechi nyingi ambazo zinakuwa na ubora kama ule wa Man City kwani timu hii imekuwa na ubora wa kipekee.

 

“Ila pia haijalishi kama tunacheza nyumbani au ugenini cha msingi sisi tunatakiwa kuwa imara na kucheza soka safi licha kuwepo kwa ugumu,” alisema Klopp.


Katika kikosi cha Liverpool baadhi ya mastaa ambao walikuwa majeruhi na wanatarajia kurejea kama Joel Matip na Naby Keita huku Thiago akikosekana.

 

Kwa upande wa Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema: “Ukiwa unacheza na timu kama Liverpool kwa wakati kama huu ni lazima utaumia na hilo tunalitambua inabidi tujipange kweli.

 

“Wote tunafahamiana vizuri tumekutana mara nyingi, zaidi dakika 90 zitasema kwani huenda yakatokea mengi na kila mmoja anataka kushinda.” City katika mchezo huo, itamkosa Sergio Aguero na Fernandinho ambao ni majeruhi.Mechi nyingine za Premier leo Jumapili ni West Brom v Tottenham, Leicester Ciy v Wolves na Arsenal v Aston Villa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top