} });
 

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiado nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga.


Maafisa wa Uhamiaji walikatas kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wa Lema kwa madai hadi wamuone Lema.


Lema alikwenda, akawaambia hana hati yake ya kusaflria kwa sababu alikuwa hasafiri, bali wanaye walikuwa wanakwenda kutafuta Shule ya Kimataifa.


Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake.


Alipovuka mpaka, Lema na familia yake walingia ndani ya gari la Mwanasheria wake George Luchiri.

Luchiri amesema alitaka ampeleke Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHRC) mara tu atakapavuka mpaka. Kwa mujibu wa UNHRC mtu anayetafuta hifadhi hahitaji kuwa na nyaraka za kumuwezesha kuingia nchi nyingine.


Aidha, Kenya imesema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema atarudishwa Novemba 09, 2020 baada ya kwenda nchini humo kutafuta hifadhi kwa UNHRC.


Lema anayeshikiliwa Kituo cha Polisi cha Kajiado amedai maisha yake yapo hatarini. Baadhi ya taarifa zinadai kuwa alikwenda Kenya kuomba hofadhi katika Ubalozi wa Marekani.

 

Hii imekuja ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia chadema, Tundu Lissu kuomba hifadhi katika Ubalozi wa Marekani kwa madai kuwa maisha yake yapo hatarini.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top