} });
 

Naibu Msajili wa Mahakakama Kuu ya Tanzania, Devotha Kamuzora akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano huo.

Jamii imeaswa kutoa wosia ili kuepusha migogoro baina ya ndugu na jamaa pindi binadamu anapofariki dunia na kwamba si kweli kwamba kufanya hivyo ni uchuro.


Hayo yamesemwa leo na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Devotha Kamuzora kwenye  semina ya ngazi ya jamii (GDSS) inayoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).


Amesema jamii huwa inadhani mtu kutoa wosia kabla hajafa ni uchuro na anaweza akafa mapema, lakini si kweli, bali ni imani potofu.


“Kila binadamu yupo safarini akielekea kwenye kifo. Ni vema kujiandaa wakati wa uhai ili pindi ukifa uache wanaobaki salama na kujiepusha na ugomvi na migogoro isiyo ya lazima.


“Ili kuepuka haya ndipo umuhimu wa kuandika na kuacha wosia unakuja na pia kipindi mtu anapofariki dunia ni muhimu kufungua shauri la mirathi mapema baada ya kifo,” amesema.


Ameendelea kusema kuwa wosia wa maandishi hauwezi kubadilishwa na wosia wa mdomo ila wasia wa mdomo unaweza kubadilishwa na wa maandishi mtoa wasia ana haki ya kuandika au kutaja sehemu tu ya mali zake kwenye wosia wake na zile ambazo hajaziandika zitasimamiwa kufuata utaratibu wa mirathi isiyo na wosia ni utaratibu unaotumika kusimamia kisheria mali za marehemu na haki za warithi.


“Mirathi imejikita zaidi kwenye kuangalia ni namna gani wategemezi au ndugu walioachwa na marehemu watamuenzi au watasimamia mali na malengo yake aliyoyapanga kabla ya kufa au kusimamia utekelezaji wa wasia aliouacha marehemu ni kwa sababu ni muhimu kufahamu juu ya uendeshaji wa mashauri ya mirathi.


“Aliyetimiza umri wa mtu mzima kisheria awe na akili timamu, anaweza akawa msimamizi wa mirathi wosia utakataliwa iwapo itagundulika kuwa wakati mtoa wosia alipokuwa anaandika akili yake haikuwa sawa kutokana na ukichaa, ugonjwa, ulevi au sababu nyingine,” amesema Devotha.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top