} });
 

KIJANA Changwa Sebeki (19) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua Kegoka Mwikwabe (22) anayedaiwa kumuondoa kwenye harusi kwa kukosa zawadi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Danilel Shillah amesema tukio hilo limetokea Oktoba 31, ambapo mtuhumiwa alimshambulia kwa kumkata na panga hadi kusababisha kifo chake.


Sababu aliyoitaja ni kuwa katika harusi moja, marehemu alikuwa anasimamia vijana wanaocheza na binti kutoa zawadi lakini mtuhumiwa alicheza na alipoambiwa atoe zawadi kama ilivyo kwa taratibu za Kikurya, hakuweza kutoa hivyo akatolewa nje.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top