} });
 


Jeshi la polisi mkoa wa Geita, linamshikilia Vestina Michael (44), mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kumtoa mimba na kumsababisha kifo Mariam Msalaba (40), ambaye alipoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa mimba nyumbani kwa mtuhumiwa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Henry Maibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kitendo hicho cha kikatili kimetokea nyumbani kwa mtuhumiwa majira ya usiku.

"Jeshi la Polisi tunamshikilia Vestina Michael, kwamba siku ya Oktoba 31 mwaka huu marehemu alifia nyumbani kwake na ndugu wa marehemu wakaleta malalamiko kwamba, ndugu yao amefia kwa mtuhumiwa wakati akimtoa mimba, hivyo tunamshikilia huyo mtuhumiwa", amesema Kamanda Mwaibambe.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top