} });
 


Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi Maafufu Bobi Wine amekamatwa na jeshi la polisi nchini Uganda akiwa katika harakati za kampeni.

Bobi wine amekamatwa na maasa wa polisi katika wilaya ya Luuka mashariki mwa Uganda,alikokuwa anatarajiwa kuendesha kampeni.

Maasa wa usalama wanamshutumu kwa kuendesha mikutano ya hadhara bila kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya homa ya Corona.  

Msemaji wa idhara ya polisi Fred Enanga ametangaza kwamba mgombea yeyote atakaye endesha mikutano ya kampeni za hadhara atakamatwa, hata hivyo haijajulikana mpaka sasa mwanamuziki huyo amepelekwa wapi na polisi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top