} });
 

 

Marafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure aliyejulikana kama Ginimbi kwa muktadha wa kijamii, wamesema atazikwa na gunia lilojaa Dola, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa "all-white funeral", kama ilivyoandikwa na gazeti la Herald.

Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.

Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji.

Familia imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima, imeripotiwa na Zim Morning post.

Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.

Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi, Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.

Wakati mwanasiasa Acie Lumumba ameahidi lita 1000 za mafuta ya dizeli, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.

Ginimbi na Maona kwa pamoja walikuwa wanatoka kwenye sherere ya "all-white" ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.

Sherehe ya Ginimbi ya kuvalia mavazi meupe maarufu 'All White Party'

Ginimbi Genius Kadungure alijulikana kama mfalme wa mitindo mbali na kufanya sherehe kubwa .

Mwaka 2010 alifanya sherehe kubwa ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo waliohudhuria walivaa mavazi meupe maarufu kama all White party mjini Harare Zimbabwe , sherehe hiyo ilizungumziwa sana mjini humo .

Miaka miwili baadaye mwaka 2012 alisimamia maadhimisho ya siku nyengine ya kuzalia kwake.

Mwaka 2013, Ginimbi aligharamia sherehe ya siku tatu katika kijiji cha kwao huko Domboshava ili kusherehekea nyumba mpya aliyojenga katika eneo hilo

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top