} });
 

 

Mpambano wa masumbwi ambao ulikuwa wa hisani, baina ya Bingwa wa zamani wa Ndodi, Mike ‘Iron’Tyson dhidi ya Roy Jones Jr umeshindwa  kumpata mbabe baada ya majaji kutangaza kuwa ni droo, mpambano huo ambao la raundi nane, ulipigwa usiku  wa kuamkia leo Novemba 29 jijini Los Angeles Marekani.

 

Mike Tyson 54 ambaye ubingwa wake wa kwanza aliupata Miaka 36 iliopita baada ya kumtwanga Trevor Berbick, Las Vegas mwaka 1986 na kuweka rekodi ya kuwa bingwa wa uzani wa juu (Heavyweight) mdogo kutwaa mkanda huo.


Muda mwingi wa pambano hilo Roy Jones alionekana kuzidiwa na makonde aliyokuwa anarushiwa na Tyson.

 

Majaji waliwashangaza wengi, baada ya kutangaza matokeo kuwa ni sare, kwani wengi walidhani Tyson ameshinda kwa jinsi alivyotawala pambano hilo ambalo halikuwa la Ubingwa 

Tyson mara baada ya pambano alisema alikuwa anaona dakika mbili ni nyingi hiyo ni kutokana kutopanda ulingoni kwa muda  kwa muda mrefu  pambano lake mwisho lilikuwa mwaka 2005 ambalo alipoteza dhidi ya Kevin McBride kwa KO na kuamua kutangaza kustaafu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top