} });
 

Polisi wa Wilaya ya Rakai nchini Uganda wanachunguza mazingira kifo cha mwanafunzi wa mwenye umri wa miaka 16, aliyekufa kwa kunywa sumu ya kuua wadudu baada ya kudaiwa kumpa ujauzito msichana wa miaka 15.

Ndugu wa marehemu, amesema kuwa kaka yake alichukua chupa ya dawa ya Paraquat, ambayo alikuwa amenunua kwa ajili ya kuua wadudu kwenye bustani yake. Alikunywa dawa hiyo na baadaye kupelekwa hospitali ambapo alikutwa na mauti siku tano baadaye.

Wazazi wa msichana huyo walikwenda nyumbani kwa kijana huyo wakisema Kenned amempa ujauzito binti yao na kutaka amuoe la sivyo watamfikisha mahakamani. Lakini pia walidadi shililngi 100,000 za Uganda kama matunzo ya kila mwezi kwa binti yao mjamzito.

Kennedy hakukubali kulipa pesa hizo kwani alikanusha kuwa na uhusiano na msichana huyo, na kusema inawezekana msichana huyo alikuwa na marafiki wengine wa kiume na hakuweza kumuoa kwani alikuwa bado kijana mdogo.

Baba wa Kennedy amesema mtoto wake alikuwa na hamu ya kuwa mhandisi na inasikitisha kwamba amekufa kabla ya kutimiza ndoto yake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top