} });
 

 

BONDIA  namba moja nchini, Hassan Mwakinyo, ametajwa kuwa bondia wa nyota tatu duniani, akihitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwamo MannyPacquiao mwenye nyota tano.

 

Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, Boxrec, jana Ijumaa, Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 dunianini kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa super welter.

 

Bondia huyo licha ya kushinda mapambano kadhaa mwaka huu likiwamo la Tshibangu Kayembe, alibaki nafasi ya 78 mpaka leo vilipotajwa viwango vipya na kupanda hadi nafasi ya 41.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top