} });
 


MAMLAKA ya Safari za Anga Marekani (FAA),  imetia saini ya kukubali kuanza  kufanya safari  kwa ndege aina ya Boeing 737 zilizopigwa marufuku kusafiri baada ya kutokea kwa ajali mbili za abiria nchini Indonesia na Ethiopia na kusababisha vifo kwa watu 346.

 

Mkuu wa FAA, Steve Dickson, ametia saini agizo linaloruhusu ndege aina ya Boeing 737 kuanza tena safari zake kwa abiria  na amesema ana uhakika wa asilimia 100 juu ya usalama wa ndege hizo.

 

Uamuzi huo wa FAA), unamaanisha ndege hizo zinaweza kuanza tena safari za abiria ifikapo mwisho wa mwaka huu.Mamlaka hiyo imetoa wito marubani kupewa mafunzo zaidi ili waweze kutumia kwa ubora wa juu kifaa kipya cha usalama kilichowekwa kwenye ndege hizo.


Aidha, wamiliki wa ndege za Boeing wamefurahishwa na hatua ya FAA na kusema kuwa wamejifunza kutokana na makosa yaliyotokea awali.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top