} });
 


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amesema kuwa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, hajawahi kutoa taarifa kama anatishiwa maisha na wala hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtishia maisha yake.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 09, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, hii ni baada ya taarifa kusambaa kwamba Lema anashikiliwa nchini Kenya, baada ya kuingia bila kuwa na nyaraka muhimu.

"Usalama wake hauko hatarini, yuko sawasawa tu na hakuna tishio lolote dhidi ya maisha yake", amesema Kamanda Hamduni.

Imeelezwa kuwa jana Novemba 9, 2020, Lema alishindwa kutoa nyaraka hizo muhimu kwa madai ya kuwa alikuwa anahofia maisha yake na kwamba alikuwa anaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kutafuta hifadhi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top