} });
 

Watu wawili wamefariki duniani baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya jana katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP James Manyama amethibitisha vifo hivyo na kueleza kuwa mmoja kati ya waliokutwa na mauti hayo ni Kijana aliyefahamika kwa jina la Yassin Khalifan 18 mkazi wa Mtaa wa Gezaulole Kata ya Gungu alipokuwa amejikinga mvua.

Manyama amesema mvua hiyo iliyoanza majira ya Saa tano asubuhi imesababisha pia kifo cha mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 aliyekutwa amefariki baada ya kusombwa na maji wakati mvua hiyo inanyesha katika Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma ujiji.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma ACP James Mnayama ameeleza mbali na vifo hivyo mvua hiyo imesababisha madhara kwa wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Jihad ambao walijerihuwa na radi na kupelekewa hospitali.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top