} });
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi  amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba Rais Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

 

Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.Uteuzi huo umeanza Novemba 08, 2020

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top